Mbolea Ya Green World – Nutriplant Organic Plus Fertilizer

mbolea ya kampuni ya green world

Kuna aina nyingi za mbolea ambazo mkulima unaweza kuzitumia katika bustani au shamba lako ili kukusaidia kupata mavuno mengi na bora zaidi. Katika mada yetu ya leo tutaizungumzia aina mpya ya mbolea inayotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Green World. Kutokana na utofauti na ubora wake, mbolea hii imepewa jina la “Fertilizer of Tomorrow.” Tofauti ya aina hii ya mbolea na nyingine nyingi ambazo hutumika kwa kuzifukia ardhini, aina hii mpya hutumika kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea na hivyo kuifanya kuwa bora kwa mmea wa aina yo yote. Kabla ya kuanza kuijadili aina hii mpya ya mbolea, hebu tujikumbushe kidogo historia ya matumizi ya mbolea kwenye nchi zetu za Afrika.

Kabla ya ujio wa wazungu, waafrika tulikwishajua umuhimu wa kutumia mbolea na mbolea za samadi ndizo zilizotumika. Baadaye elimu ilitufunza namna ya kutengeneza mbolea kwa kufukia nyasi, kinyesi cha mifugo na vitu vingine kwenye mashimo yaliyochimbwa na kuvifukua baada ya muda fulani – biwi.
Baadaye, baada ya kupata uhuru, tuliletewa aina nyingine za mbolea ambazo zilitengenezwa viwandani. Mbolea hizi zilikuwa ni za sulphates, phosphates na nitrates. Nchini Tanzania tunazijua mbolea zilizotengenezwa mjini Tanga. Kuna Single Super Phospahte (SSP) au calcium dihydrogen phospahte (Ca(H2PO4)2) na Triple Super Phosphate (TSP) ambazo hutengenezwa kutokana na mawe kutoka eneo la Minjingu-Arusha. Aina nyingine iliyozoeleka ambayo pia hutengenezwa mjini Tanga, ni Ammonium Sulphate (NH4)2SO4). Aina nyingine za mbolea, ambazo zimekuwa zikiagizwa kutoka nchi za nje, ni Ammonium Nitrate na Calcium Ammonium Nitrate.

Mbolea Ya Aina Mpya Ya Kampuni Ya Green World

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameonyesha kuwa mmea unaweza pia kupata chakula chake kupitia majani na ukawa kamilifu kabisa. Matokeo ya ugunduzi huo umetuletea aina mpya za mbolea. Mojawapo ya mbolea hizo mpya ni mbolea ya majimaji inayoitwa Mbolea - green worldNutriplant Organic Plus Fertilizer (NOPF) -fertilizer of tomorrow – inayotengenezwa na kampuni ya Green World. Mbolea hii inatunzwa ndani ya plastiki ndogo yenye ujazo wa lita moja na hutumika kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea. Utengenezaji wa mbolea hii umezingatia mahitaji yote ya mmea ikiwa ni pamoja na virutubishi vyote vinavyohitajika kwa wingi na mmea (macronutrients) ambavyo ni Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Calcium, magnesium na Sulphur, na vyote ambavyo vinayohitajika kwa kiwango kidogo (micronutrients), vikiwa ni Ferrous, Zinc, Copper, Boron, Manganese, Silicon, Molybdenum, Sodium, Cobalt na Chlorine.
Kwa vile amino acids ni muhimu katika ukuaji wa mmea, mbolea hii imejumuisha aina zote 18 za amino acids. Pamoja na ukuaji wa mmea, amino acids huupa mmea sifa nyingine nyingi sana, mfano; uwezo wa kupambana na magonjwa na wadudu, ukuaji wa haraka n.k.

Tofauti Ya Mbolea Ya Green World Na Mbolea Nyingine

Mbolea za nitrates, sulphates na phosphates hutengenezwa viwandani, kwa hiyo ni mbolea za kemikali. Mbolea hizi kiutaalamu huitwa Inorganic Fertilizers. Aina hii mpya ya mbolea inayotengenezwa na Green World, haitokani na kemikali bali na wanyama na mimea. Organic maana yake kitu kilichotokana na viumbe hai – kitu kinachotokana na mimea au wanyama. Kuna tofauti kubwa kati ya kutumia mbolea za kemikali na mbolea za organiki. Tofauti kuu ni:

1. Mbolea ya Green World ina virutubishi vyote, vile vinavyohitajika organic fertilizerkwa wingi na mmea, macronutrients, na vile vinavyohitajika kwa kiwango kidogo, micronutrients. Mbolea za kemikali hutengenezwa zikiwa na macronutrients tu.

2. Mbolea za Green World ni rafiki wa mazingira. Wakati ukiendelea kuitumia mbolea hii, mazingira yako hayaharibiki tofauti na matumizi ya mbolea za kemikali ambazo huharibu mazingira.

3. Mbolea za Green World zinatumika kwa muda mrefu na kuendela kukuletea mazao bora wakati mbolea zingine hutumika kwa muda mfupi kabla ya kuanza kudorora kwa uzalishaji.

ubora wa mazao na green world

4. Mbolea za Green World huongeza ubora wa mazao, kama ukubwa, rangi, ujazo na ladha. Mbolea nyingine za kemikali hupunguza ubora wa mazao.

5. Mbolea za Green World huboresha udongo wa shamba lako. Unaweza kuitumia kutibu ardhi iliyochoka. Mbolea hii hurudishia pH ya udongo hadi kiwango kinachohitajika na mimea cha kati ya 6-8. Mbolea za kemikali huzidisha pH ya udongo, hatimaye kuufanya udongo wa shamba lako kuwa haufai kwa mimea.

Faida Za Kutumia Mbolea Ya Green World

Uwingi Wa Amino Acids: Matumizi ya mbolea ya Green World yana faida nyingi kwenye mimea yako. Mbolea hii huupa mmea wako amino acids zote zinazohitajika na mmea ili kuufanya ukue kwa haraka, ujikinge na wadudu, usipate maradhi kiurahisi na mengineyo mengi.

Matumizi Kwa Eneo Kubwa: Mbolea hii imesheheni virutubishi vingi katika ujazo mdogo na kukuwezesha kuongeza maji mengi ili itumike kwenye eneo kubwa zaidi. Kichupa hiki cha lita 1 kinatakiwa kichanganywe na maji yenye ujazo wa lita 1,000 kiasi ambacho kinaweza kunyunyiziwa kwenye shamba la ukubwa wa hekta 6.7 au eka 16.5. Kama shamba lako ni dogo, unaweza kujaza mbolea kwenye kifuniko cha chupa hiyo ambacho kina ujazo wa ml 50 na ukachanganya na maji lita 50. Kwa kipande

kidogo cha bustani unaweza kuchangaya cc 5-10 kwenye lita 20 za maji na kunyunyizia kwenye kijieneo chako.

Salama Kwa Binadamu Na Mifugo: Mbolea ni salama kwa afya ya binadamu na mifugo. Unaweza kuchuma mboga au matunda yaliyonyunyiziwa mbolea na kuyala au mnyama akala majani yaliyonyunyiziwa mbolea bila kupata madhara.
Matokeo Ya Haraka: Mabadiliko kwenye mmea ulionyunyiziwa mbolea huoneka baada ya siku chache – siku kama 7 baada ya matumizi ya mbolea hii.

Namna Ya Kutumia Mbolea Ya Green World

Njia nyingi sana zinaweza kutumika katika kunyunyiza mbolea. Kwenye mashamba makubwa ya mboga na mimea mingine mifupi, vifaa vya kunyunyiza mbolea kama mvua kwenye eneo kubwa vinaweza kutumika. Shamba la miti ya matunda linaweza kunyunyiziwa kupitia mizizi. Drip irrigation pia inaweza kutumika kulingana na mazingira. Mtu mwenye kijieneo kidogo anaweza kutumia kifaa cha kubeba mgongoni na akanyunyiza mimea yake.

Kunyunyiza mbolea

Mbolea hii inatakiwa kuinyunyizia kwenye mimea mapema asubuhi kabla ya saa 3 au jioni baada ya saa 10. Haifai kutumika wakati wa jua kali.

Endapo baada ya kuinyunyizia mbolea mvua ikanyesha, inatakiwa kunyunyiza tena mbolea baada ya saa 24 toka mvua ilipokatika.

Mimea midogo ya mbogamboga inatakiwa kunyunyiziwa kila baada ya siku 7 hadi 10 na mimea mikubwa ya matunda kunyunyiziwa kila baada ya siku 20.

Ili mbegu ziote kwa haraka, unaweza kuloweka mbegu zako kwenye mbolea kwa saa 8 kabla ya kuzipanda.

Kutambuliwa Kwa Mbolea Hii

Baadhi ya serikali za nchi zilizopata mbolea hii siku nyingi kidogo, zimefanya utafiti wa kina kuona ubora wa mbolea hii kabla ya kuipasisha. Kwa mfano, serikali ya Nigeria kupitia wizara yake husika (Federal Ministry of Agriculture and Rural Development of Nigeria) imeipasisha mbolea hii tarehe 2 Machi 2016 baada ya wataalamu wao kuichunguza mbolea hii kwa miezi miwili katika maabara zao na kuona inafaa kabisa kwa matumizi nchini mwao. Kusoma zaidi ingia hapa:

http://en.world-food.com/news_show.php?id=849

Nchini Tanzania, mbolea hii imesajiliwa na TFRA kama Nutriplant Organic Plus Fertilizer tarehe 18/9/2017 na kupewa Certificate No. 0239 baada ya kupimwa na kuthibitika kuwa na viambato vyote kama tulivyoeleza ndani ya ukurasa huu.

Upatikanaji wa Mbolea Ya Green World

Kama umependa kutumia mbolea ya Green World kwa kilimo chako, wasiliana nasi kwa kutumia namba za hapa chini.  Unaweza pia kufanya biashara ya mbolea hii kama utajiunga na fursa ya biashara ya kampuni hii ya Green World.

Kama una maoni yako kuhusu makala hii au kama una maswali yo yote usisite kuniandikia kupitia promota927@gmail.com au kwa kujaza fomu hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kwa simu ndani ya muda wa kazi  kupitia 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.

Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biasharaa mtandao zinazotolewa na kampuni za Green World Tanzania  . Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.

Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.