Biashara ya mtandao, kama ilivyo kwa biashara nyingine yo yote, mtu huifanya ili aweze kupata mafanikio. Mafanikio katika biashara ya mtandao ni kuwa na pesa ya kumudu kununua cho chote unachokihitaji, kuwa na muda wa kutosha kufanya lo lote unalolipenda na kuwa na mtindo wa maisha unaoendana na wakati.
Mada yetu ya leo, inahusu stadi 7 ambazo unahitaji kujifunza na kuzijenga ili upate mafanikio makubwa katika biashara yako ya mtandao. Mada hii inawajibu watu wengi ambao wamekuwa wanajiuliza maswali kama; vigezo vya kufaulu kwenye biashara za mitandao ni vipi, au njia za kufanikiwa kwenye biashara ya mtandao ni zipi; au nifanye nini ili biashara yangu ya mtandao ifanikiwe?
Kwa bahati nzuri, unapohitaji kujifunza fani yo yote ya kitaalamu kama michezo, n.k., kuna stadi za msingi 7 ambazo utahitaji kujifunza na kuzimudu. Kwa hiyo hakuna jambo geni sana kwenye mada yetu ya leo.
Tuchukulie mtu anayejifunza mpira wa kikapu. Atajifunza kuudunda mpira, kulenga goli, kufanya ulinzi, stamina na vitu vingine.
Anayejifunza udereva, ataelekezwa namna ya kuwa mwangalifu barabarani, kutumia pedali, kubadilisha gia, kushika usukani na kadhalika.
Hivyo hivyo, unapoanza kumiliki biashara yako ya mtandao, una stadi za kuzijua vizuri ili uweze kupata mafanikio makubwa. Watu wengi wanaenda mbali na kufikiria makubwa sana wakati hatua zinazohitajika ni 7 tu ambazo unaweza kujifunza kirahisi na baadaye kila kitu utakachopenda kuwa nacho, utakipata bila kuumiza kichwa.
Tatizo moja ambalo huwa linajitokeza kwa wengi wanapoanza biashara ni kuwa ghafla wanaona kuwa wanafanya vitu vigeni kwao. Hali hii huwafanya wasijisikie vizuri, na kwamba hawafanyi vizuri mwanzoni, na wengi hukata tamaa. Tafadhali usifanye hivyo!
Inatakiwa kuelewa kuwa lazima kutakuwepo na “kipindi cha mpito” ambapo utatakiwa kujifunza tabia mpya na stadi mpya na kwamba unatakiwa kuvumilia hadi hapo utakapoweza.
Hapa chini ni tabia na stadi unazotakiwa kujifunza na kuzikuza katika kufanya biashara yako ya mtandao.
1. Mawasiliano Na Kuandaa Mikutano
Stadi ya kwanza kabisa kujifunza ni jinsi ya kufanya mawasiliano na watu. Huku ndiko kuitangaza biashara yako. Kuna njia nyingi za kulifanya hili ikiwa ni pamoja na kuzungumza na ndugu na rafiki, au kuwasiliana na watu walio nje ya jamii yako. Mawasiliano yanaweza kuwa ya uso kwa uso au kwa njia ya simu na siku za mwanzo unaweza kupata ugumu kidogo. Ni kitu cha kawaida kupata ugumu huo lakini cha kukumbuka tu ni kwamba utapata uzoefu na kuona ni kitu cha kawaida kadri siku zinavyokwenda. Lengo la mawasiliano haya ni kupanga muda na mahali ambapo utaweza kuwaelezea fursa uliyo nayo na kuwaacha waamue kama watapenda kushiriki au la.
Njia ya kujenga stadi hii ni kuhakikisha unafanya mara nyingi sana (mara 100 na zaidi) hadi inajengeka kuwa ni tabia yako
2. Kuwasilisha Fursa
Stadi ya pili inayotakiwa ni kuwa na umahiri wa kuielezea na kuwashirikisha watu kwenye fursa ya biashara (presenting the opportunity). Kuna utofauti wa namna ya kufanya na njia zinazotumika kutoka kampuni moja hadi nyingine, lakini mara nyingi huwa ni mawasilisho (presentation) ya dakika 20. Watu wengi hawajazoea kutoa mawasilisho mbele ya kadamnasi na inaweza kuwafanya wasijisikie vizuri siku ya kwanza. Uwasilishaji wa fursa huendelea kuwa rahisi kila siku mtu unapoendelea kuufanya na baadaye utashangaa kwa nini siku za kwanza ulisumbuka. Kumbuka tu kwamba unapoelezea fursa, unawaonyesha watu njia ya kuweza kubadilika kabisa na kuboresha maisha yao hadi kufikia kuishi maisha ya njozi zao.
Njia ya kujenga stadi hii ni kuhakikisha unafanya mara nyingi sana hadi inajengeka kuwa ni tabia yako
3. Ufuatiliaji
Kuna msemo wa wenzetu usemao, “the fortune is in the follow-up”, yaani bahati ipo katika ufuatiliaji. Kwa kawaida, watu hawajiungi mara tu baada ya kuisikia fursa. Huwa inamchukua mtu kuisikia fursa mara 7 hadi 10 kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga na fursa. Hiki ni kitu cha kawaida katika biashara. Hii ina maana kuwa itabidi kuanza kuizoea kazi ya kumkumbushia mtu kuhusu fursa yako na kuendelea naye kimazungumzo hatua kwa hatua. Ni swala linalohitaji mazoezi, uvumilivu na mpangilio. Watu wengi hawana maamuzi ya mara moja, jambo ambalo si baya.
Jinsi ya kupata stadi hii ni kuendelea kufanya hivyo kila siku hadi itakapojijenga kuwa ni tabia.
4. Kusajili Na Kuzindua Biashara Zao
Ujuzi mwingine wa kuujenga ni kuwa na uwezo wa kumzindua mwanachama uliyemsajili na kumfanya aanze kufanya biashara na kukua kibiashara katika muda mfupi iwezekanavyo. Imeonekana kuwa muda mzuri wa kuhakikisha kuwa unamzindua mtu uliyemsajili ni ndani ya saa 48 baada ya kumsajili. Ni kawaida kwa mgeni kuwa na wasiwasi pale anapoanza kitu kipya kwa sababu wanakuwa bado wana imani ndogo na kitu walichokianzisha. Kila mtu anapitia hatua hii. Kumsaidia aanze na kasi nzuri, unawajibika kuwa karibu naye mara moja. Hivyo ndivyo wote wawili, wewe na yeye, mtakapokuwa mnazijenga biashara zenu kwa haraka. Amini ninachosema……kazi itazidi kuonekana rahisi kila siku unavyoendelea kuifanya.
Jinsi ya kupata stadi hii ni kuendelea kufanya hivyo kila siku hadi itakapojijenga kuwa ni tabia
5. Kutoa Mafunzo Na Kuelekeza
Mara baada ya kumpata mtu uliyemsajili, unatakiwa kumfundisha kufanya kile ambacho wewe unakijua. Unatakiwa umpe mafunzo ya awali na kumsaidia katika kutatua vikwazo ili aanze kuona mafanikio. Wewe sasa ni mwalimu wake wa biashara unayemsaidia kupambana na vikwazo na kumweka kwenye njia sahihi ya mafanikio. Huwa ni faraja kubwa kuona kuwa mtu unayemfundisha anapata maendeleo na anaanza kutimiza ndoto zake.
Njia ya kujenga stadi hii ni kuhakikisha unafanya mara nyingi sana hadi inajengeka kuwa ni tabia yako
6. Malengo, Mipango Na Muda
Kuweka malengo, kuweka mipango ya kuyafikia malengo yako na kuwa na mpango wa matumizi ya muda wako ni stadi muhimu sana ambayo unatakiwa ujifunze, uifanyie mazoezi, uikuze na kuhakikisha unakuwa mahiri. Kama ilivyo kwa stadi nyingine nyingi, ni kitu ambacho hufundishwi shuleni. Ni kitu ambacho unatakiwa ujifundishe mwenyewe na kukifanyia kazi kila siku, wiki, mwezi na mwaka, hadi ifikie kuwa ni tabia yako. Habari nzuri ni kuwa baada ya mazoezi ya miezi 3, inapokuwa tayari ni tabia yako, kinageuka kuwa ni kitu rahisi sana kwako.
Njia ya kujenga stadi hii ni kuhakikisha unafanya mara nyingi sana hadi inajengeka kuwa ni tabia yako
7. Kujiendeleza Binafsi
Kujiendeleza binafsi ni jambo ambalo lisipofanyiwa kazi, litasababisha anguko kwenye biashara yako ya mtandao. Unapoanza biashara ya mtandao kwa mara ya kwanza, unakuwa huna ujuzi wa kufanya biashara hiyo. Hivyo, unatakawa ufanye kazi ya kujifunza. Unatakiwa uzifanyie kazi tabia ambazo hazitakikani kwenye biashara ya mtandao, utatakiwa pia ufanye kazi ya kupata stadi za biashara hiyo na mwisho uzifanyie kazi imani zako. Usitegemee vitu kuwa rahisi sana, jifunze kuwa bora kwenye biashara. Kadri utakavyokuwa unabadilika, ndivyo biashara nayo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako.
Njia ya kujifunza stadi hii ni kuhakikisha kuwa unajenga tabia ya kujifunza kila siku
Nashukuru sana msomaji wangu kwa kusoma hadi hapa chini, hii inaonyesha wazi kuwa una lengo la kupata mafanikio katika biashara yako. Mimi nakuahidi kuwa ukizingatia haya, utakamilisha ndoto zako na tutakutana ukiwa kwenye kiwango chako cha juu kabisa cha mafanikio.
Katika kurasa nyingine tutataja baadhi ya siri za mafaniko katika biashara ya mtandao na namna ya kupambana na vikwazo wakati ukiendelea na biashara hii. Kuweka malengo katika biashara ni dira ya mafaniko yako, kwa hiyo, tumeweka ukurasa mwingine kwa ajili ya kuifunza jinsi ya kuweka malengo ya biashara yako.
Usisite kutoa maoni uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza swali lo lote ulilo nalo. Ahadi yetu ni kuwa tutakujibu kwa wakati mwafaka.
Laurian.
Tafadhali tembelea blog yetu kujisomea mada mbali mbali zinazohusu biashara za mtandao na fursa za kufanya biashara za mtandao zinazotolewa na kampuni ya Green World Tanzania . Humo unaweza kuona wasomaji wengine wana maoni gani kuhusu mada zetu tunazoziandika. Pia unakaribishwa kuona video mbali mabali zinazohusu biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World kwenye channel yetu ya YouTube.
Kutembelea blog bofya HAPA.
Kutembelea channel yetu ya YouTube bofya HAPA.