Dunia ya sasa imekuwa na mabadiliko makubwa katika ufanyaji wa biashara. Makampuni makubwa ya kutoka nchi zilizoendelea yamegundua kuwa yanaweza kufanya biashara kwa wepesi na vizuri zaidi kwa kuwaruhusu watu binafsi kunadi na kuuza bidhaa zao. Makampuni hayo katika kufanya hivyo yanaondoa gharama kubwa za kutangaza bidhaa zao kwenye vyombo vya habari na kuwaachia wanachama waliojiunga na kampuni hizo kufanya kazi hiyo. Mwanachama anatakiwa kutoa kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kifurushi cha kuanzia na anunue angalau kiasi kidogo cha bidhaa kila mwezi, hivyo kumwezesha kuanza biashara kirahisi na kutafuta kiasi kidogo sana cha pesa kama mtaji wa biashara yake. Hii ni aina ya biashara ya mtaji mdogo sana ambayo nitaizungumzia katika mada yetu ya leo.
Biashara ya aina hii huitwa biashara ya mtandao – Multi-Level Marketing (MLM) au Direct Selling. Kuna maoni mengi mno kuhusu aina hii ya biashara, wapo watu wengine wakilisikia tu hili neno – biashara ya mtandao- linawachefua. Watakuambia hizi ni biashara za kitapeli au ni biashara za watu walioshindwa maisha na maneno mengine mengi. Napenda leo tujue maana ya biashara ya mtandao na ukweli wake kuhusu kumsaidia mtu anayetaka kuanza biashara kwa mtaji mdogo.
Nini Maana Ya Biashara Ya Mtandao (Network Marketing)
Biashara ya mtandao ni mfumo wa biashara ambapo mwakilishi wa kampuni husika anapata mafao kutokana na mauzo yake binafsi na mauzo ya watu aliowashawishi kujiunga na kampuni hiyo na kuwafundisha mfumo wa biashara yake.
Biashara za mtandao hutoa kipato endelevu (Residual Income), maana yake ni kuwa mwanachama anaendelea kulipwa pesa muda mrefu baadaye kwa kazi aliyoifanya mara moja. Kwa mfano, mwanachama aliyemshawishi mteja kununua bidhaa fulani na yule mteja akatoa oda ya kupewa ile bidhaa kila mwezi, mwanachama huyu atalipwa mwezi ule ambao mteja aliinunua ile bidhaa na kila mwezi baadaye ili mradi mteja yule ataendelea kununua bidhaa ile.
Biashara za mtandao humlipa mwanachama wake kutokana na mauzo yanayofanywa na wanachama walioingizwa kwenye kampuni hiyo kwa kupitia jina lake. Kampuni hizi hutofautiana, kampuni nyingine humlipa mwanachama hadi kiasi fulani tu cha ngazi za chini yake, wakati kampuni nyingine hazina ukomo wa ngazi za chini ya mwanachama huyo.
Kama mwanachama aitwaye John atawashirikisha Amina, Grace na Doreen kujiunga na kampuni, na Amina akawashawishi Juma na Lilian, John atakuwa na wanachama watatu wa ngazi yake ya kwanza ambao ni Amina, Grace na Doreen na katika ngazi yake ya pili atakuwa na Juma na Lilian. Vivyo hivyo, John ataendelea kujenga timu kubwa chini yake. Kampuni itamlipa John kutokana na juhudi zake binafsi (direct income) na kutokana na mauzo yanayofanywa na timu iliyo chini yake (Leveraged Income).
Isitoshe, kampuni hizi hutoa zawadi nyingi kwa wanachama wao wanaofanya vizuri. Kuna zawadi ndogo ndogo na zawadi kubwa ambazo ni pamoja na safari za kwenda nchi za nje gharama zote zikilipwa na kampuni, zawadi za magari na hata nyumba kubwa za kifahari.
Faida Za Biashara Ya Mtandao
Kuna faida nyingi sana zinazopatikana kutokana na mwanachama kushiriki katika biashara za mtandao. Nitajaribu kuelezea chache hapa chini:
Mtaji mdogo: Biashara hizi huhitaji mtaji mdogo sana wa kipesa, nyingine hukuwezesha kuanza biashara kwa kiingilio kidogo sana, pengine kama Tshs 24,000/= tu na nyingine zikitaka utoe laki chache za shilingi kama kiingilio na kifurushi cha kuanzia. Hazina masharti na ukiritimba wa kutaka vitambulisho na wadhamini. Kampuni hizi zinataka tu uwe na nia ya dhati ya kufanya biashara. Unaweza kufika kwenye kampuni na muda huo huo ukajisajili na kuanza biashara.
Hakuna gharama za uendeshaji: Biashara nyingine zote ambazo tumezizoea zinataka ukodi chumba cha biashara, ukate leseni ya biashara na vitu vingine vingi. Biashara ya mtandao haidai kuingia gharama hizi. Karibu kila kitu, pamoja na zana za kazi, zinagharimiwa na kampuni, kazi yako wewe ni kusambaza bidhaa tu.
Wewe ndiye Bosi: Hizi ni aina ya biashara ambayo haina mtu wa kukufuatilia mambo yako, wewe ndiye bosi wa biashara yako – ni biashara ya kujiajiri mwenyewe. Maamuzi yote na mipango yote ya kibiashara yanakuwa juu yako wewe mwenyewe, hakuna mtu wa kukusukuma au kukufokea. Utajipangia ni muda gani ufanye kazi na muda gani upumzike, ukizembea umekosa kipato na ukifanya kazi umepata kipato.
Hakuna ukomo wa kipato: Tofauti na kazi za kuajiriwa, biashara hizi hazina ukomo wa kipato, mwanachama atapata kipato kulingana na ujuzi wake wa kazi, juhudi zake za kazi na muda anaoutumia kufanya biashara yake. Wapo watu walioacha kazi baada ya kuona wanapata kipato ambacho ni mara dufu ya kile alichokuwa akipata wakati akiwa katika ajira.
Kipato endelevu: Mwanachama analipwa muda mrefu baadaye kwa kazi aliyoifanya mara moja, mara nyingine miaka mingi tu baada ya kuifanya ile kazi mara moja. Mwanachama akipata mteja mmoja wa kudumu, anakuwa amepata kipato cha kudumu, awepo asiwepo au yeye afanye kazi au asifanye kazi, kipato chake kipo pale pale. Hii ina msaada sana pale unapopata dharura au kuumwa na huwezi kushiriki kwenye biashara.
Biashara ya kimataifa: Biashara ya mtandao inakuruhusu kupata kipato kwa kazi ya mwanachama aliye nje ya nchi yako ili mradi tu wewe ndiye uliyemhusisha akaanza kuifanya biashara na kampuni yako. Kwa hiyo, utapata pesa kutokana na kazi inayofanywa na mtu aliye mbali na wewe na pengine nje ya nchi yako.
Biashara ya kurithisha: Kampuni nyingine zinamruhusu mwanachama kumrithisha biashara yake mtu anayemtaka yeye. Faida kuhusu hili na pale umri unapokuwa haukuruhusu tena kuendelea na pilikapilika za mitaani au kwa bahati mbaya mwanachama akapatwa na umauti. Mtu aliyeteuliwa ambaye anaweza kuwa mtoto wake, ataendelea kunufaika na matunda aliyopanda mwanachama aliyefariki.
Biashara Za Mtandao Ni Za Kweli?
Biashara za mtandao ni za kweli na ni halali. Nimeandika ukurasa tofauti kabisa kuhusu hoja hii kutokana na urefu wake. Hapo utaweza kuona historia ya biashara ya mtandao na watu maarufu duniani waliojihusisha na biashara hizi. Kutokana na ukweli wa biashara hii, raisi wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, alipata kuizungumzia. Raisi Donald Trump ni mtu ambaye ameifanya sana akishirikiana na rafiki yake, bilionea Robert Kiyosaki. Unaweza kusoma zaidi kuhusu hili kwenye ukurasa wa “Kuna Ukweli Gani Katika Biashara Ya Mtandao?”
Biashara za mtandao hazina tofauti na vitu vingine tunavyokutana navyo katika maisha, kama hukufanya utafiti wa kutosha kabla ya kujiunga, unaweza kuishia kwenye kampuni mbovu na mwisho wa siku ukawaambia watu kuwa biashara za mtandao si za kweli. Kuna makampuni ya watu wahuni ambayo yameshafika hapa nchini na kuwalaghai watu na kuna kampuni bora ambazo kila siku watu wananufaika nazo. Ukichagua kampuni yako vizuri, ukaielewa na kufanya kazi kwa juhudi, hakuna sababu ya kushindwa kubadili maisha yako. Kuna vigezo vya kuangalia kabla ya kuchagua kampuni ya kufanya nayo kazi ambavyo nilijaribu kuvielezea katika ukurasa wa “Namna Ya Kuchagua Kampuni Ya Mtandao“.
Kuchagua kampuni yako vizuri pekee hakukupi maendeleo tayari. Kampuni unayofanya nayo kazi inahitaji ipate faida kutokana na biashara yake, hakuna kampuni itakayokuja hapa kugawa hela – kamwe haitatokea. Lazima uuelewe vizuri mpango wa kibiashara wa kampuni “Compensation Plan” kwa kuhudhuria mafunzo na kuwasilikiza waliokutangulia (Upline Members). Kuna vitu vingi vya kuzingatia katika kufanya biashara yako ili upate maendeleo, lakini kwa bahati nzuri vyote ni vya kitabia na si vya kutumia pesa. Soma mada yetu kuhusu hili hapa “Siri Za Kufanikiwa Katika Biashara Za Mtandao“.
Kwa kutoa mfano tu, hapa nchini namfahamu dada mmoja ambaye alisomea ukunga (midwifery) akaacha kazi na kuanza kuuza duka la dawa pale Tabata (Dar). Akapata kusikia kuhusu kampuni moja ya kuuza madawa (Green World Tanzania) akaanza kununua dawa katika kampuni ile na kuwatibia wagonjwa wake kwa kutumia dawa za kampuni ile. Baadaye akaamua kuwa mwanachama kabisa wa ile kampuni (mwaka 2014).
Umependa kujua zaidi au kujiunga na biashara ya mtandao ya kampuni ya Green World? Wasiliana nasi kwa njia moja uipendayo kati ya hizi hapa chini:
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.