Habari
Biashara ya mtandao ni kwa kila mtu. Lakini, si
kila mtu anaweza kufanya biashara ya mtandao.
Ni ukweli usiofichika kwamba hii ni biashara ya
kushangaza ambayo inamwezesha mtu ye yote kuweza
kuwa tajiri bila kujali kuwa ametokea kwenye ukoo
wa matajiri au la, bila kujali elimu ya mtu au
ukubwa wa mtaji wake. Inamwezesha mtu ye yote hata
yule aliyetokea kwenye familia ya kimaskini ambaye
hakujulikana kabisa.
Faida za biashara hii ni nyingi. Ni biashara isiyo
na ukomo wa kipato, inayokuwezesha kusafiri po pote,
inakuwezesha kuifanya nchi yo yote (ukiwa kwako),
na kukuruhusu kuwasaidia watu wengine wapate
mafanikio wakati ukijiimarishia mafanikio yako.
Inakuwezesha kujipatia umaarufu na marafiki kutoka
kona zote za dunia, kujipatia zawadi za magari ya
kifahari, nyumba za kifahari na hundi za pesa
nyingi. Inakuruhusu kuishi maisha ya kisasa na
ya kipekee.
Lakini bado, si kila mtu anaweza kufanya biashara ya mtandao …
Kwa Nini?
Kwa sababu inahitaji mtu mwenye tabia na maono ya
namna fulani. Kwa hiyo, wakati nawashauri watu
kujiunga na biashara hii, kila mtu anatakiwa
afanye tathmini yake binafsi kuona kama ataiweza
au aendelee na mfumo mwingine uliozoeleka wa
kuajiriwa na kufanya kazi za 9/5; yaani saa 9 kila
siku, siku 5 kwa wiki. Jitathmini na jipe majibu
ya kweli.
Ikiwa wewe ni aina ya watu wale ambao wamezoea
kufanya kazi kwa kusukumwa na bosi, kuelekezwa na
kupangiwa kila kitu cha kufanya, kama si mtu wa
kujituma, na kama wewe si mtu wa kupenda
kujiendeleza …. hii si fani yako!
Na kama ni mtu uliyekwishalemaa na kusubiri
mshahara wa kila mwisho wa mwezi, hapa patakushinda.
Biashara ya mtandao inataka mtu mwenye mawazo ya
kijasiriamali. Si kila mtu ana mawazo hayo.
Mjasiriamali hasubiri mshahara aliopangiwa mwisho
wa mwezi, bali bonasi kubwa inayotokana na kazi
aliyoifanya. Kama wazo la kupima na kuona uwezo
wako wa kuzalisha linakusisimua, kama umechoka
kabisa kupunjwa na kupangiwa kiasi cha kupata ili
uendeshe maisha yako, biashara ya mtandao
inakukaribisha.
Biashara ya mtandao ni kwa mtu anayejiamini na
mwenyewe dhamira ya kushika dira ya maisha yake
mikononi mwake. Ni kwa mtu jasiri anayeamini kuwa
hatma ya maisha yake iko mikononi mwake na
kamwe haipangwi na mtu mwingine ye yote yule awaye.
Kwa hiyo unahitajika kuwa mtu mwenye nafsi
inayojiamini, uwe na ari ya kufanya kazi, uweze
kuendesha kazi zako bila kusimamiwa na kuwa
mahiri katika ufuatiliaji. Pia unahitajika kuwa
mwerevu. Kwa nini werevu ….
Mafanikio ya biashara ya mtandao ni kuwa na uwezo
wa kuendeleza namna ya kupata mafanikio kutoka
kizazi kimoja hadi kingine (Duplication).
Sehemu kubwa ya ufanyaji wa biashara hii ni
kunukuu njia za mafanikio zilizobainishwa na
kampuni na watu walio juu yako waliokwisha pata
mafanikio. Haina maana wewe huna uwezo wa kubuni
njia zako, lakini kwa nini uanze kufanya
majaribio wakati vitu vilivyojaribiwa na
kuthibitishwa kuwa vinafaa na ambavyo watu
wengi wamevitumia na kufanikiwa vipo?- why waste
your time re-inventing the wheel?
Wafanya biashara werevu hujifunza kwanza njia
hizi zilizokwisha wasaidia wengine wa juu katika
biashara zao na baadaye wakaweka nyongeza zao.
Hii huwapa dhamana ya kuanza biashara na kuanza
kuona mafanikio bila kuyumba.
Kama kila wakati utataka uifanye biashara hii
kwa njia zako mwenyewe, biashara hii itakuwa
ngumu kwako. Utajifanyia vitu unavyovipenda
lakini hutapata mapato ambayo yanatokana na
watu uliowasajili (passive income).
Kama mjasiriamali mwingine ye yote lazima uwe
jasiri katika kupambana na changamoto na
kuwashinda watu wanaokufahamu wataokushinikiza
kuiacha biashara yako. Unachokifanya wewe ni
kitu tofauti na wengi wanaokuwa na hofu na
vitu wasivyovielewa vizuri. Wapo watakaokutilia
shaka, wengine watakukatisha tamaa na wapo
watakaokuonea wivu. Kwa hiyo utakapowaambia
kuwa sasa unafanya biashara ya mtandao ili
kuboresha maisha yako, usishangae pale kila
mmoja atakapokuja na neno lako. Wapo watakao
kushauri kwa sababu zao uachane nayo,
watakaobeza na kusema hutaiweza. Utatishwa
na kutolewa mifano kede kede ya watu
walioshindwa na kupata hasara. Wengine
watayasema hayo wakiwa na dhamira nzuri tu,
lakini bahati mbaya, watakuwa wanatoa
ushauri kwenye vitu aambavyo hawana ufahamu
navyo.
Watu wengi hawana nia kabisa ya kuwa matajiri.
Wamekuzwa kuwa na kiwango kidogo cha
kujitambua. Bila wao wenyewe kujitambua akili zao
zinawafundisha kuamini kuwa hawastahili
kufanikiwa katika maisha. Wana imani kimakosa
kuwa kuna nguvu za mizimu zinazoongoza umaskini
wao na kwao kufanikiwa itahitaji kazi
ya ziada nje ya uwezo wao.
Watu hawa ndio wengi na ndio wanaotuzunguka.
Na, hakuna kitu kinachowasumbua watu hawa
zaidi ya kuoa\na mwenzao wanayemfahamu anapata
mafanikio. Watajitahidi kufanya wawezalo
kukuzuia katika njia yako ya mafanikio, hata
kukuhujumu kama ikibidi. Kufikia mafanikio
yako lazima uwe imara, na usitegemee ushauri
wa wengine – ni maisha yako!
Unapohitaji kupata ushauri, jambo la busara
ni kumtafuta mtu ambaye tayari alikwisha fanya
biashara na kufanikiwa. Tabia ya kupata
ushauri kutoka kwa watu waliokwisha fanikiwa
itakuongezea uwezekano wa wewe pia kufanikiwa.
Jambo jingine muhimu katika kufanikiwa katika
biashara ya mtandao ni kuwa na uaminifu,
uadilifu na uelewa mkubwa. Unapomshirikisha mtu
kwenye biashara hii na kumweka chini yako,
unakuwa mshirika wake kibiashara na mshauri
wake maisha yote. Hata akijifunza mbinu za
biashara na akapata mafanikio na kuwa moja ya
vinara wa juu, bado watakutazama kama dira
yao ya uadilifu, uwajibikaji na utamaduni wa
kampuni yenu. Tofauti na mfumo wa biashara
wa zamani, biashara ya mtandao hutegemea
kuaminiwa kwa mmsajili (sponsor) na wanachama
walio chini yake.
Kuaminiwa na uadilifu ndiyo rasilimali yako
kuu kwa watu uliowasajili na kuwaongoza
kwenye biashara ya mtandao. Mamilioni ya watu
wamechoshwa na ubovu wa mahusiano, umbeya, siasa
mbaya na kukosa uwajibikaji kwenye kazi za
ajira. Uaminifu, uwajibikaji na kuishi kama
jamii moja ndani ya biashara za mtandao ni
vitu vitakavyomvutia zaidi mtarajiwa wako
kuliko hata pesa, magari na safari za nje.
Unaposema uongo kwa mtu wa chini yako – hata
kama ulifikiri ingemsaidia na kumvutia –
unakuwa umeharibu dhamana ya msingi kwa
biashara hii. Wale waliopata mafanikio ya
ya kudumu katika biashara hizi, ni wale
walioishi kwa maneno yao.
Biashara ya mtandao inataka kuwa na au kujenga
uwezo wa kufundisha. Hapa ni kwa nini….
Katika jamii zetu, asilimia yapata 10 ya
watu wanaweza kuuza bidhaa. Wanapenda kuuza
bidhaa na wanaipenda kazi hiyo; hawaogopi
kuambiwa HAPANA. Asilimi 90 ya watu, kuambiwa
hapana ni kitu ambacho hawapendi kukisikia na
kinawafanya wakose raha. Ukiwafundisha watu
kuanza kuwapigia simu watu wasiowajua (cold calling),
kuwagongea milango watu wasiowajua au
kuwafuata watu wasiowajua mitaani, utakimbiza
asilimia 90 ya watu uliowasajili na utawajibika
kila siku kusajili wengine.
Hawewezi kujiona wanayafanya mambo haya….
Ukweli ni kuwa ni mtu mmoja tu kati ya
1000 anayeweza kumudu biashara hiyo ya
kuzungumza na watu wageni kabisa. Ni kipaji cha
kipekee. Kwa hiyo, kama wewe una kipaji hicho
na ukafundisha hivyo, utashindwa kuendeleza
ujuzi wako kwa watu wa chini yako na utakosa
kipato kutokana na watu wa chini yako – residual
na leveraged income.
Mfanya biashara ya mtandao mahiri anawafundisha
watu wake stadi chache, rahisi ambazo kila
mmoja anaweza kuzimudu na kuzifundisha kwa
watu wa chini yake. Kitu cha kwanza ni kuona
kuwa kila mtu wa chini yake ameelewa stadi
hizo na anaweza kuzifundisha. Kwa jinsi hii,
jumuia yake itakua haraka. Siri ya kukua
haraka kibishara kwa hiyo ni:
Ongoza kikundi kikubwa cha watu, wanaofanya
kila wakati vitu vichache, kwa kipindi kirefu.
Si ajabu kuona kuwa walimu, maprofesa, walimu
wa michezo, wakufunzi wengine na watu wanaofanya
kazi kwenye makundi makubwa ya watu, wanaimudu
sana biashara ya mtandao. Kwa hiyo kama una uwezo
wa kufundisha, una nafasi nzuri sana kupata
mafanikio ya haraka katika biashara ya mtandao.
Hatuwezi kufunga somo letu la leo bila kuelezea
umuhimu wa kujiendeleza binafsi. Kwa walio wengi,
asubuhi mapema kabla watoto hawajaamka, huwa
ni muda mzuri wa kufanya tafakari kuhusu biashara
yako na kujiendeleza. Unahitaji kuwa na maktaba
ndogo na kanda za video za kukupa ari na
kurudisha jicho lako liangalie kwenye njia
yako moja nyoofu uliyoamua kuifuata.
Kwa kusoma hapa leo naamini umeona mwenyewe kuwa
biashara ya mtandao ni tofauti sana na kazi au
biashara za makampuni. Kwa kifupi, unatakiwa
kuwa na mwamko wa kijasiriamali, kujituma, uwe
mwaminifu, ukubali kuacha mapenzi na matakwa ya
nafsi yako na ufuate misingi iliyokwishafanyiwa
utafiti.
Baada ya maelezo hayo kuhusu biashara unayotegemea
kuifanya, nakuruhusu sasa ujitafakari na kutoa
maamuzi yako binafsi. Endapo unajiona kuwa ni mtu
ambaye utaweza kuungana nasi, bofya juu ya sentensi
hiyo hapo yenye maandishi mekundu.
Tafadhali usibofye hapa chini kama hiki si kitu ulichodhamiria kukifanya!
NAPENDA KUFANYA BIASHARA HII
Laurian 0756 181651
Green World – Machinga Complex Office, Dar Es Salaam.