Green World Tanzania – Fursa Bora Ya Biashara Ya Mtaji Mdogo

Kampuni ya Green World Tanzania ni moja ya makampuni mengi ya mtandao ambayo yameingia hapa nchini kwetu Tanzania. Kampuni hii ilisajiliwa hapa kwetu mwaka 2009 na tangia hapo kuna baadhi ya watanzania ambao wameshanufaika sana na kampuni hii. Mimi nafikiri niseme neno moja tu kwamba watanzania bado hawajaielewa vizuri kampuni hii na kwa hiyo hawajaitumia fursa hii ipasavyo. Mimi binafsi naamini kuwa hii ni fursa ya kipekee kama mtu ataielewa vizuri. Katika mada hii nachambua kwa nini nafikiri hii ni fursa iliyo bora kuliko nyingi zilizopo ili mtu aweze kutoa maamuzi yaliyo sahihi kuhusu kujiunga nayo.

Kujiunga na Green World ili unufaike na fursa ya biashara, endelea kusoma HAPA>.

Kama nia yako ni kujiunga na Green World ili uweze kupata bidhaa za kampuni hii kwa bei ya punguzo la asilimia 20 tu bila kujihusisha na biashara ya mtandao, yaani unahitaji kuwa mwanachama mlaji, endelea kwa kubofya HAPA>

Kwa Nini Green World Ni Fursa Bora Ya Biashara Tanzania?

Kwa sababu si kila fursa ni bora kwa kila mtu na kwa kila nchi, tuangalie kwa nini Green World ni bora kwa walio wengi waishio Tanzania. Hapa chini ni sababu za msingi kwa hoja yangu:

chakula baada ya mkutano

Kianzio au Kifurushi cha Kuanzia Green World Tanzania: Kampuni hii haina kifurushi cha kuanzia bali ina kiingilio kidogo cha Tshs 35,000/= tu, hii ni kama leseni yako ya kukuwezesha kufanya biashara na kampuni.  Kwa kulipa kiingilio hiki utakuwa tayari mwanachama kamili wa kampuni ya Green World Tanzania. Utapewa:

  • Kadi yenye namba ya uanachama wako wa kampuni
  • Tovuti za mafunzo ya biashara ya mtandao
  • Kitabu cha orodha na maelezo ya bidhaa za kampuni na  mpango wa malipo wa kampuni.
  • Tovuti ya kufanyia biashara yako. Tovuti hii itaonyesha manunuzi unayoyafanya, wanachama waliojiunga chini yako na manunuzi yao na bonasi yako uliyoipata katika mwezi huo wa kazi.
  • Fursa ya kuhudhuria mafunzo ya kibiashara BURE. Mafunzo hayo ni ya kwenye madarasa, kupitia whatsapp na online ZOOM trainings.

Kadi utakayopewa ni ya kimataifa, maana yake ni kwamba po pote duniani utakapoionyesha kwenye ofisi ya Green World, utapokelewa na kupata huduma zote muhimu. Unaweza sasa kuanza kuchagua bidhaa unazozipenda na kuzinunua muda wo wote. Utauziwa kwa bei ya uanachama ambayo ni asilimia 20 pungufu ya bei ya reje reja. Kila mmoja wetu anamudu kutoa kiingilio hiki, hili sina shaka nalo.

Bidhaa zinazohitajika na jamii na kuuzika: Bidhaa za kampuni hii ni virutubishi vya mwili vya kusaidia kuweka afya za jamii kwenye hali bora au watu kuondoa matatizo mbalimbali ya kiafya. Kampuni hadi sasa ina bidhaa za aina tofauti zaidi ya 100. Bidhaa ni nyingi kwa ajili matatizo ya kipekee ya watoto, akina mama, wanaume na binadamu kwa ujumla. Bidhaa hizi zimethibitishwa na FDA (Food and Drugs Administration) ya Marekani na TFDA ya Tanzania. Watu wengi wamezitumia  na kuthibitisha  kuwa ni bora katika ufanyaji wake wa kazi na wengi huwaambia ndugu zao pia kuhusu ubora wa bidhaa hizi.

Kwa vile kila siku watu wanahitaji kuboresha afya zao, soko ni kubwa sana na kila siku linazidi kupanuka. Hapa nchini Tanzania pekee, kuna shuhuda nyingi za watu waliohangaika kwa miaka mingi na kupona kupitia bidhaa zetu.

Bei za Bidhaa za Green World Tanzania: Bei za bidhaa za kampuni hii zimepangwa hivi kwamba kila mwananchi aweze kuzimudu na kuifanya biashara yake kuwa na wateja wengi wa kununua bidhaa.

Ulipaji wa kampuni ya Green World Tanzania: Kampuni humlipa mwanachama mafao yake kila mwezi bila kukosa na kwa wakati.

Mpango Wa Biashara (Compensation Plan). Mpango wa biashara wa kampuni ya Green World umeandaliwa kuwa rahisi kueleweka kwa kila mtu na rafiki kwa watu wa rika na viwango mbalimbali vya kipesa. Umeandaliwa ili mtu aweze kupanda daraja kiurahisi na kwa kila tendo analolifanya. Kampuni haina kumteremsha mtu daraja alilofikia, hata kama kwa bahati mbaya mwanachama alishindwa kufanya biashara kwa miezi kadhaa, akirudi ataendelea kwenye ngazi ile ile alipoachia.  Green World haina ukomo wa vizazi chini yako vitakavyochangia kwenye kipato chako hivi kwamba unaweza kupata mafao (Leveraged Income) kutoka kwenye kundi kubwa  sana  la wanachama chini yako .

Kampuni ya kuaminika: Kampuni hii ipo kwenye biashara kwa miaka mingi, toka mwaka 1993, na ipo katika nchi zaidi ya 70 ulimwenguni – Afrika peke yake ina ofisi katika nchi tofauti 33. Kampuni ina makao yake makuu Michigan, USA,  ambako pia kuna vituo vya utafiti 8 kwenye vyuo vikuu tofauti, vikiongozwa na Cornel University. Raisi wa kampuni, Dr Deming Li, ni msomi mwenye shahada ya uzamifu kwenye somo la microbiology,  anayeheshimika na kutumiwa na taasisi mbalimbali duniani. Hii ni uthibitisho tosha kuwa hii si kampuni ya kuja kuchukua hela za watu na kutoweka kama yalivyofanya baadhi ya makampuni. Ukijiunga na Green World, unajenga biashara ya kudumu. Kupata ushahidi zaidi unaweza kuingia kwenye website – www.world-food.com.

MWANACHAMA LAURIAN MWAJOMBE AKIWA SAFARINI KIBIASHARA
MWANACHAMA  AKIWA SAFARINI KIBIASHARA

Utanufaika Vipi Kwa Kujiunga Na  Kampuni  Ya Green World Tanzania?

Kampuni ya Green World inawakaribisha watu wote kujiunga na kunufaika kutokana na huduma zinazotolewa na kampuni bila kujali elimu zao, vipato vyao au nafasi zao katika jamii – ni kwa ye yote. Unakaribishwa kujiunga ili uchague kati ya yafuatayo:

  1. Mwanachama Mlaji: Unaweza kujiunga ili kupata mafunzo ya afya na kununua bidhaa kwa bei ya punguzo la asilimia 20 tofauti na bei ya rejareja. Kwa kujiunga utaweza kununua bidhaa kutoka kwenye duka la Green World kwa kutumia kadi yako. Utachagua bidhaa unayoipenda na utanunua idadi unayoitaka bila masharti yo yote. Hii itakusaidia kulinda afya yako, ya ndugu zako na marafiki. Faida ya ziada, ni kwamba baadaye (baada ya kununua bidhaa zinazofikia 500,000/=), utapewa bonasi kwa manunuzi utakayoyafanya katika mwezi, bonasi ambayo inaanzia asilimia 20 ya manunuzi yako. Unanuna bidhaa na kupata pesa mwisho wa mwezi …….. jambo la kipekee!  Wewe utaitwa ni mwanachama mlaji.

Huhitaji kujenga timu? – La hasha!

Kama mwanachama mlaji hutatakiwa kutoa ada yo yote ya mwaka wala mwezi. Unajiunga mara moja tu na utaendelea kupata huduma kwa bei nafuu milele. Hakuna masharti ya bidhaa gani ununue wala kiwango cha kununua, unanunua unachokipenda, wakati unaotaka mwenyewe. Ni fursa ya kipekee ya kuboresha afya yako!

Kama unapenda kuwa mwanachama mlaji, pata maelezo zaidi kutoka ukurasa wetu wa Jiunge Na Green World Kuboresha Afya Yako.

Unaweza kuviona vifurushi (packages) vya bidhaa za Green World hapa:

Vifurushi Vya Green World

2. Biashara Ya Rejereja: Unaweza pia kujiunga ili kufanya biashara au kujiajiri. Unaweza kuwa mfanya biashara mdogo wa rejareja au mfanya biashara mkubwa wa rejareja uliyefungua duka lako au kituo chako cha afya. Uamuzi ni wako.

3. Network Marketer: Unaweza kuchagua kufanya biashara ya mtandao kama ukipenda. Maelezo zaidi kuhusu biashara za mtandao utayapata katika mada nyingine ndani ya tovuti hii. Kwa kifupi ni kwamba utawashirikisha wengine kujiunga na kampuni na hivi utajenga timu chini yako. Kampuni itakulipa kwa kazi unazozifanya binafsi na kutokana na asilimia ya mauzo yaliyofanywa na watu walio chini yako. Faida ya hili ni kuweza kupata kipato endelevu (residual income) kwa tendo la siku moja na kipato kitakachotokana na juhudi zako za kuleta watu na kuwafundisha (leveraged income.) Hatimaye utapata kipato kikubwa sana kwa kazi ndogo sana utakayokuwa unaifanya na kuwa umefikia uhuru wa kipesa.

Kampuni ya Green World Tanzania imejengwa kwa kutumia mfumo wa 3*3 Matrix maana yake ni kwamba ukijiunga unaweza kuchagua kunufaika na bonasi zinazotokana na kazi zinazofanywa na watu wengine kwa  kuwashawishi angalau watu watatu kujiunga chini yako. Hao watatu wa mwanzo ni ngazi yako ya kwanza ya mtandao wako unaoujenga. Hao watatu wa chini yako utawalea na kuwafunza wawashawishi angalau watu watatu kila mmoja. Wakifaulu kufanya hivyo, wewe utapanda ngazi na kupata mafao zaidi. Wale tisa nao inabidi wapate watu watatu watatu kila mmoja ndipo utakapopanda ngazi zaidi na kupata mafao makubwa zaidi. Kampuni hii haina ukomo wa ngazi za chini yako, maana yake haina ukomo wa mapato – ukomo wa kipato hapa ni ukomo wa juhudi zako.

Ngazi Za Wanachama Wa Green World 

Kampuni ya Green World ina ngazi kwenye hadhi za Consultants, Managers, Directors na ngazi ya juu kabisa ni Honorary Chairman. Unapojiunga kwa kutoa kiingilio chako, tayari unakuwa kwenye ngazi ya kwanza ya Consultants, utaitwa 1*C (One  Star Consultant). Utaendelea kupanda ngazi hadi kufikia 8*C.

Ukifanya mambo yako vizuri utaingia kwenye hadhi nyingine ya u-Manager. Hapa kuna One-Star Manager hadi Three-Star Manager.

Baada ya ngazi hizi za mameneja unaingia kwenye hadhi ya Directors ambapo unaanza na gazi ya One-Star Director na kuishia kwenye ngazi ya Five-Star Director.

Ngazi ya juu kabisa ya kampuni ya Green World Tanzania ni Honorary Chairman.

Mafao Ya Green World Tanzania

Sasa tulizungumzie lile lililokufanya uingie kwenye internet na kuanza kupekua, yaani kampuni ya mtandao ambayo ni nzuri kujiunga nayo-Mafao au Malipo na marupurupu. Najua hili ndilo ulilokuwa unalitafuta muda wote, kwani sababu kubwa ya kuhangaika na makampuni haya ni kujiongezea kipato au kupata ajira na kubadili maisha. Kampuni ya Green World itakupa si nyongeza ya kipato tu bali itakupa ajira ya kudumu ukipenda. Ni biashara ya kukupa shughuli ya kudumu isiyo na ukomo. Kuna jambo ambalo pengine hujawahi kulisikia kwenye makampuni mengine -“Ukishajenga biashara yako na Green World Tanzania ikakua, unaweza kumrithisha ye yote yule endapo utaishiwa nguvu za kuendelea na biashara hii au kupoteza maisha. Kwa hiyo kujenga biashara na kampuni ya Green World ni sawa na kuwekeza kwenye jengo au kitu kingine cho chote kikubwa kisichohamishika.” Upo hapo?

Kampuni ya Green World Tanzania inatoa mafao na marupurupu kwa njia 6 tafauti:

  • Retail profit
  • Direct Bonus
  • Indirect Bonus
  • Leadership bonus
  • Honorary Bonus
  • Special Awards
safarini SA
WANACHAMA WA GREEN WORLD SAFARINI KUHUDHURIA MKUTANO JOHANNESBURG

Retail Profit au faida ya biashara ya rejareja: Rejea maelezo yetu hapo juu ambapo tulisema ukishajiunga na Green World utanunua bidhaa kwa bei ya kampuni. Unaweza kuziuza bidhaa hizo kwa bei za rajareja kwa wateja wako na kupata faida. Kampuni ya Green world inakuruhusu kufungua duka na ukauza bidhaa hizi pia katika duka lako- Kazi kwako ndugu yangu unayetafuta ajira au njia ya kuongeza kipato.

Direct Bonus: Ukianza kujenga mtandao wako utalipwa kutokana na manunuzi unayoyafanya wewe binafsi kutoka kwenye kampuni. Malipo haya yatategemea ngazi uliyopo na kiasi cha bidhaa ulizonunua. Kwa mfano, ukiwa 3*C, utapewa asilimia 20 ya manunuzi yako kama direct bonus.

Indirect Bonus: Hii ni asilimia ya mauzo ambayo kampuni  itakulipa wewe kutokana na manunuzi yaliyofanywa na watu ambao umewasajili kwenye kampuni. Hii inategemeana na ngazi aliyopo mtu uliyemsajili.

Leadership Bounus: Hii ni tunu endelevu unayopewa mwanachama kwa kujenga na kuisadia timu yako.

Honorary Bonus: Honorary bonus hutolewa kwa wanachama waliofikia hadhi ya Distributor ambapo hupewa asilimia ya pato lote la kampuni la dunia.

Special Awards: Hizi ni tunu ambazo utapewa na kampuni kwa kufikia malengo fulani yaliyowekwa na kampuni. Kwa mfano, ukifikia ngazi ya 6*C katika kipindi cha miezi 6, utapewa fursa ya kutembelea na kuzuru nchi ya China kwa wiki mbili, gharama zote zikiwa juu ya kampuni.

WANACHAMA KUTOKA TANZANIA - MRS MBUYA, MCHUNGAJI BOAZ NA G.MBUYA - HOTELINI JOHANNESBURG
WANACHAMA KUTOKA TANZANIA – MRS MBUYA, MCHUNGAJI BOAZ NA G.MBUYA – HOTELINI JOHANNESBURG

Mfano wa pili, ni pale utakapofikia ngazi ya 7*C katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja ambapo utatunukiwa gari lenye thamani ya $ 10,000 ( Tshs milioni 20 za Tanzania.)  Kuna tunu kubwa zaidi za kufikia kupewa Villa yenye thamani ya $150,000 (Tshs milioni 300 za Tanzania.)

ZAWADI MAGARI GREEN WORLD
VIDEO YA SHEREHE YA KUPEWA ZAWADI ZA MAGARI, UBUNGO PLAZA 2015. WANACHAMA 4 WALIPEWA MAGARI.

Umependa Kujiunga Na Kampuni Ya Green World?

Kujiunga na kampuni hii soma kwanza ukurasa wa kabla ya kujiunga  na Green World, kisha fuata maelekezo. Mwandishi wa mada hii nitazungumza na wewe moja kwa moja, usikate tamaa endapo mawasiliano yatachelewa kidogo. Unaweza  pia kuijiunga kwa kubonyeza juu ya maneno  JIUNGE SASA kwenye picha ya hapa juu kisha kufuata maelekezo.

Kwa maswali au maoni kuhusu mada hii, wasiliana nasi kupitia promota927@gmail.com au jaza fomu yetu hapa chini kwenye ukurasa huu. Vilevile  tunapatikana kwa simu ndani ya saa za kazi kwenye namba 0655 858 027 au 0756 181 651. Nje ya Tanzania anza na code  +255  kisha namba, mfano +255756181651 .