Watu wengi wamekuwa wakibabaika wanapokabiliwa na watu wanaowafuata na kuwashawishi kujiunga na kampuni za mitandao au pale wanapokuwa wameamua kwa mapenzi yao kuingia kwenye biashara za mtandao wasijue namna ya kutoa maamuzi sahihi kwamba ni kampuni ipi au zipi ndizo bora kujiunga nazo. Kwa maoni yangu, hii ndiyo hatua muhimu kuliko zote kwa sababu endapo utaangukia kwenye mikono ya kampuni mbovu, nguvu zako na mtaji wako vyote ni bure.
Leo katika ukurasa huu tutaona vigezo vya kuvitumia katika kuchagua kampuni ya mtandao ya kujiunga nayo. Moja kwa moja nitaanza kwa kuviorodhesha vigezo hivyo au sifa za kampuni bora na kuvitolea maelezo.
1. Historia Ya Kampuni
Zipo kampuni ambazo zinaanza biashara na baada ya muda mfupi zinapotea au kufilisika. Kama ulikuwa mmoja wa wanachama wa kampuni ya namna hiyo, lazima utakuwa umeathirika kwa namna fulani. Inabidi upate kampuni ambayo ina historia ya kufanya biashara kwa muda mrefu (angalau miaka 5), kwa ufanisi na ambayo biashara yake bado inaendelea kukua na si ile ambayo imefikia ukomo. Hii ni muhimu kwa sababu asilimia 90 ya makampuni yanayoanzishwa hufa katika miaka 2 ya kwanza. Njia rahisi ya kupata taarifa hii ni kupitia internet ingawa kuwauliza ndugu na marafiki wengine inaweza kusaidia pia.
Unatakiwa kuhakikisha kuwa kampuni yako ina ofisi zinazoeleweka na kuna anuani kamili ili kujiridhisha kuwa unafanya biashara na kitu kilicho hai na kuwa utaweza kupata msaada pale utakapouhitaji.
Yafaa vile vile kuchunguza historia ya mmiliki wa kampuni hiyo ili kujua tabia zake na wadhifa alio nao. Kuna watu wengi wajanjawajanja wanaoanzisha kampuni na baada ya muda mfupi kuziacha na kuanzisha nyingine na kuacha madeni na wanachama wake wakiwa yatima. Wengine hawana sifa zinazotosha kuendesha makampuni waliyoyaanzisha.
Pia inatakiwa ufanye uchunguzi kujua jinsi kampuni ilivyofanya kazi zake toka ilipoanzishwa. Utahitaji kujua kama haikuyumba kimtaji na kwamba ina rekodi nzuri ya mahusianao na watu na makampuni mengine na kama ilikwaruzana na wengine, jinsi ilivyojitahidi kupata suluhu. Kampuni bora itapata cheti cha AAA kinachotolewa na taasisi moja ya nchini Czech. Vile vile unaweza kuichunguza kampuni yako kwa kuingia BBB (Better Business Bureau) ambamo utapata takwimu za kampuni yako. Ingia google na kupata reviews za kampuni uliyokusudia kuungana nayo, hapa utapata maoni mengi ya watu ambao tayari walishafanya kazi na kampuni hiyo. Utapata taarifa hizo kwa kuandika jina la kampuni na kisha reviews.
2. Bidhaa Za Kampuni
Kampuni bora ya mtandao ni ile ambayo bidhaa zake zinalenga kutatua matatizo ya wateja katika jamii unayoishi na zimethibika kufaulu katika kufanya hivyo. Bidhaa ambazo zitatangazwa halafu zikashindwa kukidhi mahitaji ya wateja zitakuwa na muda mfupi sana wa mauzo kabla ya wateja kugundua kuwa haziwafai. Bidhaa zitakazokidhi haja ya wateja zitakurahisishia kazi wewe mwuzaji kwani baadaye zitajiuza zenyewe. Bidhaa hizo pamoja na kutatua matatizo ya wateja ziwe na bei ambazo wateja wengi wataweza kuzimudu kwani pamoja na ubora wake bidhaa ambayo bei yake itakuwa juu mno itauzika kwa wateja wachache sana wenye uwezo. Kumbuka kuwa wewe kama mwuzaji utanufaika zaidi pale utakapouza bidhaa kwa wingi zaidi.
Kama kampuni yako inauza bidhaa za kuboresha afya ya binadamu, chunguza kama zimethibitishwa na FDA (Foood And Drug Administartion) ya Marekani na kama zimepasishwa na TFDA ya hapa Tanzania. Na kama ni bidhaa za aina nyingine, basi ziwe zimepasishwa na chombo husika cha kundi hilo la bidhaa, kwa mfano, mbolea iwe imepasishwa na TFRA, n.k. Endapo bidhaa zako hazitakuwa zimepasishwa, utashindwa kuzifanyia matangazo kwenye vyombo au sehemu zilizo za wazi kama kwenye mitandao, vyombo vya habari, maonyesho makubwa n.k. na hivyo kukupunguzia uwezo wa kuziuza kwa wingi.
3. Mpango Mzuri Wa Ulipaji (Compensation Plan)
Mpango mzuri wa ulipaji na ambao ni rahisi kuuelewa ndio utakaokupa wewe pesa. Kama kampuni haina mpango mzuri wa ulipaji kamwe hutapata pesa ya kutosha na kama mpango wao si rahisi kueleweka utakosa pesa nyingi kwa sababu ya kutojua namna ya kuitumia kampuni yako vizuri. Kwa vile ulijiunga na kampuni ya mtandao ili upate pesa ya kuboresha maisha yako, kitu cha kwanza cha kutazama ni mpango wao wa ulipaji na kuusoma au kuupitia kwa makini. Hili ndilo kosa ambalo watu wengi hulifanya, kujiunga na kampuni na kuanza kuchakarika bila kuujua kwa undani mpango wa ulipaji wa kampuni yake.
4. Msaada Wa Zana Za Kazi Na Mafunzo
Ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na uendelee kibiashara kwa muda mwafaka kampuni nzuri itatoa baaadhi ya zana za kufanyia kazi na mafunzo bure. Zana ambazo zitakusaidia ni pamoja na tovuti, picha kwa ajili ya matangazo ya kampuni, mikanda ya video, vipeperushi na hata matangazo ya maandishi ambayo yameandikwa kiutaalamu. Kampuni nzuri hutoa mafunzo ya kila mara bila gharama yoyote.
Watu wengi walio mashuhuri kwenye biashara wanazungumza kuwa kampuni yenye mafunzo bora ndiyo kampuni bora zaidi. Wanaendelea kusema kuwa, kitu kikubwa katika maisha yako si kupata pesa tu sasa hivi, bali kupata mabadiliko ya kimaendeleo katika nafsi yako (personal development.) Unahitaji kubadilika kifikra na kuwa kufikiri kama mjasiriamali, unahitaji kubadilika kiimani na kuamini katika biashara unayoifanya, kubadili tabia zako nyingi zisizofaa na kujenga uwezo wa kuwaongoza watu. Watu hawa mashuhuri wanasema, “ili upate pesa zaidi, unahitaji kuwa na mabadiliko zaidi ya kimaendeleo kwenye nafsi yako.” Hakuna maendeleo katika nafsi dhaifu. Kwa hiyo, kampuni inayotoa mafunzo ya kukuendeleza kinafsi ndiyo kampuni inayokupa nafasi ya kupata maendeleo.
5. Pambanua Kati Ya Biashara Ya Mtandao Na Pyramid Schemes
Kampuni ya biashara ya mtandao lazima ina bidhaa zake na wanachama wake ni lazima wazisambaze bidhaa hizo ili wapate pesa. Hakuna pesa bila kazi, kamwe! Kampuni inayokutangazia kuwa utapata pesa bila kuuza bidhaa, inakudanganya, ni namna ya utapeli. Kamwe hakuna kampuni itakayokupa pesa bila kazi, zote zimeanzishwa ili kupata faida. Jiulize, utapataje pesa bila kazi, wao watazipata wapi?
Pyramid schemes ni aina ya biashara ambapo pesa huwa ndiyo bidhaa, na ni biashara haramu. Kwetu hapa unaweza kuilinganisha na UPATU.
Nakushauri uusome ukurasa wa “Jee, Biashara Ya Mtandao Ni Ya Kweli?” ili uweze kuifahamu historia ya biashara hii na misingi ya ufanyaji wake kazi. Pia utaweza kujua kwa undani tofauti kati ya pyramid schemes au ponzi schemes na biashara hii, na kusikia wafanya biashara mashuhuri na baadhi ya marais wakiizungumzia biashara hii.
Ndugu msomaji hivi ni baadhi ya vigezo muhimu vya kuangalia unapotaka kujiunga na kampuni ya mtandao ili ufanye biashara. Hapa kwetu yapo makampuni mengi sana, ya zamani, na kila siku makampuni mapya yanaingia. Ukitumia vigezo hivyo hapo juu, utakuwa umejiweka kwenye nafasi nzuri sana ya kupata kampuni bora ya mtandao ya kufanya nayo biashara. Unaweza kusoma maelezo ya kampuni chache ambazo mimi binafsi nazipendekeza kuwa ni bora kwenye kurasa za ” Kampuni Ya kirutubisho Cha Trevo” na “Kampuni Ya Green World Tanzania“.
Video hii hapa chini inamwonyesha mama Hanisha alivyoweza kuchagua kampuni ambayo hatimaye imempa mafanikio makubwa kiafya na kimapato:
Pia nimeandika kuhusu siri za kupata mafanikio katika biashara za mtandao ambazo watu wengi waliofaulu wamezitumia. Unaweza kuzisoma kupitia ukurasa huu “Siri Za Kufanikiwa Katika Biashara Za Mtandao.”
Kama una maoni yoyote kuhusu mada hii, usisite kuniandikia. Nitafurahi sana kupata fursa ya kukujibu.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.
Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651 au 0768 557606.