Ukurasa huu ni muhtasari wa bidhaa za Green World kwa kufuata matatizo katika mwili wa binadamu. Bidhaa zinazotumika kusaidia kuondoa tatizo katika eneo moja, zimekusanywa pamoja ili kuwa mwongozo wa haraka haraka katika kutoa huduma.
Muhtasari huu huongeza bidhaa kila wakati kwa sababu kampuni yetu inaendelea na utafiti na kila wakati inatoa bidhaa mpya.
Kujua jinsi ya kuweza kununua bidhaa za kampuni hii kwa matumizi binafsi, rejea ukurasa wetu wa “Jiunge na Green World, kuboresha afya yako.”
Kifurushi Cha Afya Ya Mifupa Na Maungio Ya Mifupa
Kwa kawaida hatupati matatizo ya mifupa na maungio ya mifupa mara moja, lakini bado unaweza kupunguza uwezekano wa kutokea kwa kubadili mtindo wa maisha. Unaihitaji mifupa ili kufanikisha shughuli zako za kawaida- unaihitaji kufanya shughuli muhimu mwilini mwako:
. Kulinda viungo vya ndani ya mwili wako
. Mifupa, maungio ya mifupa, tendoni kwa pamoja hukuwezesha ufanye miondoko mbalimbali
. Uboho, ndani ya mifupa mirefu hutengeneza chembechembe za damu
Ni Nini Hutokea Usipotunza Mifupa Yako Na maungio Ya Mifupa Yako?
Mifupa kukosa uimara, maumivu kwenye joints kubwa kama mgongoni, kwenye nyonga au magoti, rheumatoid arthritis, maumivu kwenye maungio madogo ya mikono, viwiko, na gout.
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya mifupa na maungio ya mifupa:
Joint Health Plus Capsule
Compound Marrow Powder
Calcium Softgel
Kidney Care Capsule
Cordyceps Plus Capsule
Multi-Vitamin
Kifurushi Cha Kupunguza Unene Na Uzito Wa Mwili
Sababu kubwa ya kulinda uzito (unene) wa mwili wako ni za kiafya na si mwonekano. Unene huongeza uwezekano wa kupata magonjwa mengi ya mwili na kiakili kama; kisukari, high blood pressure, mafuta kwenye ini, mafuta ndani ya damu, matatizo ya mishipa ya moyo, matatizo ya mishipa ya ubongo, matatizo ya mfumo wa upumuaji na huweza kufupisha maisha kwa kiwango kikubwa sana. Kwa wastani, unene hufupisha maisha kwa miaka 6 hadi 7. Tatizo hili la unene limekuwa moja ya matatizo
makubwa sana ya kiafya duniani, kwa watoto na wakubwa katika karne hii ya 21.
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha unene wa mwili:
Pro-slim Tea
Slimming Capsule
Lipid Care Tea
Meal Cellulose
Intestine cleansing Tea
Chitosan Capsul
Kifurushi Cha Afya Ya Mwanamke
Mwanamke mwenye afya ni mrembo. Kuanzia siku ya kuzaliwa hadi siku ya mwisho, afya yako na tabia zako za kike huendeshwa
na homoni zako, mabadiliko katika homoni hizo yakiamuru kwa kiwango kikubwa mambo yatakayokutokea katika maisha yako:
Matatizo kabla ya hedhi
. Tumbo kujaa
. Kunenepa mwili
. Kuwa na hasira
. Kutotulia kimawazo
. Maumivu ya kichwa na/au mgongo
. Kusikia njaa kali/kupenda kula
. Uchovu wa mwili
. Maziwa kujaa
. Wasiwasi
. Kutojisikia vizuri au kuwa na mfadhaiko
Matatizo kwenye maziwa
. Uvimbe ulio tofauti na sehemu nyingine za ziwa au usioondoka
. Ngozi yenye magamba kuzunguka chuchu
. Kubadilika kwa umbo la ziwa
. Kujitokeza kwa vijishimo kwenye ngozi ya ziwa
. Mabadiliko kwenye chuchu kama kurudi ndani
. Kutokwa uchafu kwenye chuchu na hasa ukiwa na damu
Kupungukiwa damu
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya mwanamke:
Maumivu Kabla Ya Hedhi (PMS
Soy Power Capsule
Carefree Capsule
Baada Ya Kukoma Hedhi
Soy Power Capsule
Calcium Softgel
Compound Marrow Powder
Carefree Capsule
Multi-Vitamin Tablet
Matatizo Ya Maziwa
Multi-Vitamin Tablet
Deep Sea Fish Oil Softgel
Vitamin E
Kupungukiwa Damu
Spirulina Plus Capsule
Pine Pollen tea
Royal Jelly Softgel
Kifurushi Cha Afya Ya Ubongo
Unaikumbukaje njia ya kurudia nyumbani? Unafikiri kivipi? Unawezaje kuzungumza na wenzako? Kwa nini unakuwa na hisia mbalimbali ? Matendo haya yote yanatokana na ufanyaji kazi wa ubongo wako … kitovu cha mfumo wa neva katika mwili wako. Cerebellum huratibu pozi na miondoko yako. Brainstem huendesha upumuaji, mapigo ya moyo, na shughuli nyingine. Cerebrum hukuwezesha kufikiri, kujifunza na kumbukumbu.
Magonjwa na matatizo mengi yanayoathiri ubongo huwa ni huanza taratibu na ukubwa wake huongezeka na umri. Kushindwa kujitambua na kupoteza uwezo wa akili humathiri mtu na familia yake kwa kiwango kikubwa.
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya ubongo:
Ginkgo Biloba Plus Capsule
Deep Sea Fish Oil Softgel
Soybean Lecithin Softgel
Blueberry Super Nutrition
Compound Co-Q10 Capsules
Multivitamin Tablet
Kifurushi Cha Afya Ya Mwanamme
Matatizo mengi ya Kiafya yanawahusu watu wote, wake kwa waume. Lakini kuna baadhi ya matatizo ambao yanawahusu wanaume peke yao. Matatizo haya ni pamoja na Tezi Dume, Ugumba na matatizo ya kushindwa kukamilisha tendo la ndoa. Wanaume wapo hatari kubwa zaidi ya kuumia, vifo kwenye ajali za barabarani na kujiua. Pamoja na changamoto hizi za kiafya, huwa ni wagumu kuwaona ni watu wa kuvipuuza viashiria hivi, ni wagumu kuwaona madaktari ili kupata ushauri na ni wazito kuomba
msaada wanapoona mabadiliko kwenye miili yao. Baadhi ya matatizo yanayowakumba wanaume wa rika tofauti ni:
Jogoo kushindwa kuwika
. Uume kushindwa kusimama kabisa
. Uume kusimama ukiwa dhaifu
. Uume kusimama kwa muda mfupi sana
Kuwahi kufika kileleni
Matatizo ya tezi dume
. Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
. Mtiririko dhaifu wa mkojo
. Kukojoa kwa shida
. Kujisikia kuwa hujamaliza mkojo
. Mkojo kuendelea kudondoka kwa muda mrefu baada ya kumaliza
. Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
. Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kwenda haja ndogo
. Maambukizi ya wadudu kwenye njia ya mkojo
. Kushindwa kukojoa ghafla
. Matone ya damu katika mkojo
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya mwanamme:
Kidney Care for Men
Cordyceps Plus Capsule
Vigpower Capsule
B-Carotene & Lycopene Capsule
Prostasure Capsule
Ginkgo Biloba Capsule
Kifurushi Cha Afya Ya Macho
Macho ni mlango wa fahamu ulio wa muhimu kuliko mingine yote katika mwili wa binadamu kwani ndio unaotuwezesha kuiona dunia hii ilivyo nzuri. Tunatumia macho yetu kutofautisha rangi na vyanzo mbalimbali vya mwanga. Wenzetu wanasema “eyes are the soul windows” – macho ni milango ya nafsi zetu kuonyesha umuhimu wa macho. Lakini huwa hawatambui umuhimu wa macho hadi siku watakapopoteza uwezo wa kuona.
Macho huweza kupata matatizo kutokana na sababu nyingi zikiwemo ukavu, miwasho, pink eye, mtoto wa jicho, glaucoma, myopia, hypermetropia n.k.
Kisukari Na Matatizo Ya Macho
Matatizo ya macho kutokana na kisukari ni moja ya magonjwa mapya yatokanayo na kisukari na tatizo linaloongoza kwa kuwaletea upofu watu wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 74. Kisukari huweza kuathiri hadi sehemu 4 za macho yako; lensi, optic nerve, vitreous na retina kutokana na kuharibiwa kwa mishipa ya damu na uwingi wa sukari na pressure ya juu.
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya macho:
Blueberry Juice
Blueberry Eye Care Softgel
Multi-Vitamin Tablet
Zinc Tablet
Vitamin C
Vitamin E
B-Carotene & Lycpene Capsule
Deep Sea Fish Oil Softgel
Kifurushi Cha Afya Ya Mfumo Wa Mmeng’enyo Wa Chakula
Jee, unajua ni namna gani unaweza kuyamudu maisha yako kila siku? Unawezaje kufanya kazi, kucheza, kufanya mazoezi au kufanya shughuli nyingine? Unapata wapi nishati ya kukuwezesha kuzifanya shughuli hizo? Bila shaka, ni kutoka kwenye chakula unachokula. Wakati wa kumeng’enya chakula mwili wako unafyonza virutubishi mbalimbali vinavyotoa nishati ya kuviwezesha viungo kufanya shughuli zao. Mmeng’enyo wa chakula unafanywa na viungo vingi vikiwa ni pamoja na mdomo, koo, mfuko wa tumbo la chakula, utumbo mwembamba, utumbo mpana, rectum, mkundu na viungo vingine kama ini na kongosho. Kazi kuu ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni kuvunja vunja wanga, protini na mafuta na kuwa molekuli ndogo.
Matatizo Ya Mfumo Wa Mmeng’enyo Wa Chakula
Gastroesophageal Reflex Disease (GERD)
vidonda vya tumbo
kuziba choo
Ini
Ini ni kiungo kikubwa kuliko vyote vya mwili. Ini lipo sehemu ya juu ya kulia ya tumbo, mara nyingi chini ya mbavu. Ni kiungo pekee katika mwili wa binadamu kinachoweza kujikarabati baada ya kupoteza tishu zake. Ini lina wigo mpana wa shughuli ikiwa ni pamoja na kutoa sumu mwilini, ujenzi wa protini, na kutengeneza kemikali nyingine muhimu katika kumeng’enya chakula.
Kongosho Kisukari na insulin.
Kifurushi Cha Kutoa Sumu Mwilini
Kifurushi Cha Afya Ya Kinga Za Mwili
Kwa nini kinga za mwili ni muhimu kwa afya yako?
Katika mwili wako kuna mfumo wa kinga wa ajabu unaoitwa Kinga Za Mwili. Kazi ya mfumo wa kinga za mwili ni kuwatambua maadui wa mwili na kuwaangamiza. Maadui hawa ni pamoja na seli za mwili zenye dosari pamoja na vitu kutoka nje, kama bakteria, virusi, vimelea na sumu ambavyo hupenda kuushambulia mwili wako.
Matatizo ya kawaida yanayotokana na dosari za kinga za mwili:
1. Rhematoid arthritis
2. Multiple Sclerosis
3. Type I Diabetes melitus
4. Allergy
5. Primary Biliary Cirrhosis na Autoimmune Hepatitis
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha kinga za mwili:
Multi-Vitamin Tablet
Spirulina Plus Capsule
Vitamin E
Vitamin C
Compound Marrow Powder
Calcium Softgel
Zinc Tablet
Se Tablet
Protein Powder
Deep Sea Fish Oil
Compound Co-Q10 Capsule
Bluberry Juice (High Vc)
Blueberry Super Nutrition
Kuding Tea
Green World Energy Tea
Pine Pollen Tea
Propolis Syrup/Capsule
Royal Jelly Capsule
Ganoderma Plus Capsule
Cordyceps Plus Capsule
Ginseng RHs Capsule
Kifurushi Cha Afya Ya Moyo
Mfumo wa mzunguko wa damu huundwa na moyo na mishipa ya moyo ikihusisha arteri, veni, kapilari ambavyo husambaza damu na mfumo wa tezi za limfu ambao husambaza limfu. Hufanya kazi kusambaza virutubishi kama acidi za amino, gesi, homoni, seli za damu n.k. kwenda na kutoka kwenye seli ili kupambana na magonjwa na kusaidia kuweka joto la mwili kwenye kiwango kinachotakiwa.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani inaonyesha kuwa idadi ya vifo na ulemavu vinavyotokana na matatizo ya moyo na mishipa ya moyo kwenye nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la Sahara ilipanda kutoka miliono 5.3 kwa wanaume na milioni 6.3 kwa wanawake mwaka 1990 na kufikia milioni 6.5 na milioni 6.9 ilipofika mwaka 2000, na inaweza kupanda hadi milioni 8.1 na milioni 7.9 ifikapo 2010.
Atherosclerosis – ugonjwa wa arteri na kisababishi cha magonjwa ya moyo ya Angina na mshituko wa moyo.
Bidhaa za Green World za kusaidia kulinda na kuboresha afya ya moyo:
Cardio Power Capsule
Blood Cleanse Capsule
Lipid Care Tea
Deep Sea Fish Oil Softgel
Ginkgo Biloba Plus Capsule
Compound Co-Q10 Capsule
Vitamin E
Vitamin C
Multi-Vitamin Tablet
Garlic Oil Softgel
Kifurushi Cha Kujilinda Na Saratani
Ripoti mpya ya International Agency for Research on Cancer (IARC) inaonaisha ukubwa wa tatizo la kansa duniani, ugonjwa ambao utaweza kuwa chanzo nambari moja cha vifo duniani ifikapo 2010. Shirika la Afya Duniani (WHO) linatabiri kuwa vifo kutokana na saratani vitazidi kuongezeka, na kukadiria vifo milioni 12 ifikapo 2013.
Ni Zipi Dalili Na Viashiria Vya Kansa?
Inakupasa kujua dalili za kawaida na viashiria vya kansa. Kumbuka kuwa kuona cho chote katika hivi ina maana kuwa tayari una saratani – vitu vingine vingi vinasababisha dalili hizi. ukiona dali hizi na zikadumu kwa muda mrefu au kuzidi kuwa mbaya, tafadhali mwone mtaalamu wa afya.
Kupungua uzito ghafla kusiko na sababu Homa isiyi na chanzo maalumu Uchovu Mabadiliko ya rangi ya ngozi au miwasho
Dalili Na Viashiria Vya Baadhi Ya Aina Za Kansa
Pamoja na dalili za kawaida za hapo juu, inatakiwa kuwa makini na dalili nyingine ambazo zinaweza kuashiria saratani. Yafaa kutoa angalizo kuwa dalili hizi zinaweza kuwa zimesababishwa na vitu vingine. Yafaa kumwona daktari kupata uhakika mara moja.
. Mabadiliko katika utoaji haja kubwa au ndogo
. Madonda ambayo hayaponi
. Madoa meupe ndani ya mdomo au vijialama vyeupe juu ya ulimi
. Mwanamke kutokwa damu au uchafu ukeni kusiko kwa kawaida
. Uvimbe kwenye maziwa au sehemu nyingine za mwili
. Matatizo wakati wa kumeza
. Kikohozi sugu au sauti ya kukwaruza
Nafasi Gani Mlo Kamili Unachukua Katika Kutibu Kansa?
Wagonjwa wa kansa wanahitaji kupata mlo bora wakati wakiendelea na tiba. Mlo wanaoupata ndio utakaoamua hatma ya maisha yao.
Wakati tiba ikiendelea mwili hupambana kwa nguvu zake zote kuziua seli za kansa, na kujaribu kuzikarabati na kuzibadilisha seli zilizoharibiwa na tiba ya kansa. Mlolongo wa kazi hii ni mgumu sana kwa hiyo mwili unahitaji kiasi kikubwa cha virutubishi ili kuzirudisha shughuli za mwili kwenye kiwango kinachotakiwa.
Bidhaa za Green World za kusaidia kujilinda na saratani:
Multi-Vitamin Tablet
Zinc Tablet
Blueberry Juice (High Vc)
Se Tablet
B-Carotene & Lycopene Capsules
Deep Sea Fish Oil Softgel
Bidhaa za Green World za kusaidia kujitibu saratani
Meal Cellulose
Garlic Oil Softgel
A- Power Capsule
Ganoderma Plus Capsule
Spirulina Plus Capsule
Blueberry Super Nutrition.
Kifurushi Cha Afya Ya Mfumo Wa Upumuaji
Tunatumia mfumo wa upumuaji unaohusisha njia za hewa, mapafu na misuli, kuingiza oksijeni ndani ya mapafu na kutoa nje carbon dioxide na kiasi kidogo cha oksijeni.
Uchafuzi wa hewa na magonjwa ya mfumo wa upumuaji
Kuwepo kwenye mazingira kwa muda mrefu ya uchafuzi wa hewa kupitia moshi wa magari, moshi kutoka kwenye mitambo (mashine) mbalimbali, mitambo ya kuchoma taka, na mitambo ya uyeyushaji huongeza hatari ya magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama mzio, pumu, chronic pulmonary diseases na saratani ya mapafu.
TB: Maelezo, Viashiria na Dalili
TB ni ugonjwa wa kuambukiza wa mapafu unaojitambulisha kwa kukohoa, homa, kukonda, kukohoa damu, udhaifu wa mwili na kuchoka na maumivu ya kifua. Husababishwa na bakteria TB bacilli kupitia hewa.
Milipuko ya Ugonjwa na kutosikia dawa (drug resistance):
Bara la Afrika ndilo lenye vifo vingi zaidi vya TB. Isitoshe, ndilo bara ambako watu wengi zaidi wanapata maambukizi kwa sbabu kinga zao za mwili zinadhoofishwa na madawa yanayoharibu kinga, kutozingatia mattumizi ya dawa, au UKIMWI.
Kushindwa kuzingatia masharti ya matumizi ya dawa kunaweza kusababisha viungo vya miili kufikia hali ya kushindwa kusikia dawa tena. Tatizo la hali ya miili kutosikia dawa za TB limekuwa likiongezeka duniani. kwa hiyo, vita dhidi ya TB inategemea kinga za sindano na kuizuia kwa kuboresha mfumo wa kinga za mwili.
Pumu
Pumu ni ugonjwa sugu unaonekana mara nyingi unaoathiri njia za hewa wenye dalili za kujirudiarudia za kupumua kwa shida, kifua kubana, kuishiwa pumzi, kukohoa usiku au mapema asubuhi.
Chanzo
Karibu nusu ya pumu ni ya urithi na nusu inayobaki hutokana na sababu za mazingira kama vile uchafuzi wa hewa kutokana na uwingi wa magari, viwanda, moshi wa sigara, vumbi, taka na hewa ya ndani isiyo safi n.k.
Kujaribu kuzuia vishababishi (allergens) wakati ukiinua kinga za mwili ndiyo njia kuu ya kuzuia kujitokeza kwa pumu.
Kikohozi sugu
Kikohozi sugu ni kile kinachodumu kwa wiki tatu au zaidi, na mara nyngi hutokana na tatizo jingine.
Kuzuia kikohozi sugu
. kukwepa mazingira ya moshi . badili chakula, kwepa caffeine ipatikanayo ndani ya kahawa, chai na soda . kiweke kichwa chako na sehemu ya juu ya mwili juu ya mto ulalapo . acha kuvuta sigara
Kifurushi Chh Green World Cha Mfumo Wa Upumuaji
. .